Saturday, March 09, 2024

SERUKAMBA AWAAGA WATENDAJI MKOANI SINGIDA KWA KUWAAGIZA MIRADI YOTE KUKAMILIKA KWA WAKATI

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, leo tarehe 9 Machi, 2024 amehamishiwa kutoka Mkoa wa Singida kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Omar Dendego, kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida huku akiwaagiza watendaji kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.

Kwa muujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 09 Machi, 2024 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi, ikieleza mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri imeeleza kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza leo tarehe 09 Machi, na uapisho wa Wakuu wa Mikoa utapangwa baadaye. 

Akiwa katika kikao cha kamati ya ushauri wa Mkoa (RCC) kilichofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Serukamba, ghafla alionyesha tabasabu na shahuku ya kuongea jambo huku wajumbe nao wakionesha tabasabu kwa kile kilichokuwa kimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kikihusisha uteuzi na uhamisho huo.

Mara baada ya muda mfupi ndipo Serukamba aliposhindwa kuvumilia na kuamua kuwaambia wajumbe wa kikao hicho kwamba amehamishwa kutoka Mkoa wa Singida na kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Omar Dendego, kuhamia Mkoa wa Singida.

Aidha, Serukamba, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kumuamini katika nafasi hiyo na amemuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha anawatumikia Wananchi hao wa Mkoa wa Singida kikamilifu.

Hata hivyo Serukamba, amewashukuru Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Singida, akianzia na Katibu Tawala Mkoa huo Dkt. Fatuma Mganga kwa ushirikiano aliyokuwa akiupata, watumishi wote wa Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi, Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi wote kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, wajumbe wa kikao hicho wamempongeza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo kwa katika kipindi chote cha uongozi wake Mkoani hapo wakisema hakika amekuwa ni kiongozi aliyekuwa akisukuma maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wanasingida kwa ujumla hasa katika suala la kilimo cha utumiaji mbolea.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akionyesha tabasabu lake muda mfupi mara baada ya kuonekana kuendelea kuaminiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati alipokuwa kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).









No comments:

Post a Comment