MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amemwagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Singida kuwapangia wakuu wa idara kila
mmoja kusimamia mradi mmoja inayotekelezwa hivi sasa na wawe wanatoa taarifa ya
maendeleo ya ujenzi kila siku ili iweze kukamilika haraka kabla ya Juni 30
mwaka huu.
Ametoa agizo hilo jana (Mei 29, 2023) baada ya kutembelea na
kukagua miradi 12 katika Halmashauri ya
Wilaya Singida na kubaini miradi inayotekelezwa wameachiwa walimu, Wenyeviti wa
vijiji na watendaji wa vijiji na kata kuisimamia pekee yao hali iliyosababisha baadhi
kasi ya ujenzi kusuasua.
Serukamba ambaye aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa
Singida (RAS), Dkt. Fatma Mganga, alisema Serikali imeleta fedha nyingi kwenye
Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hivyo isimamiwe kwa ukaribu
viongozi na wananchi waendelee kuhamasishwa kujitolea nguvu kazi ili iweze
kukamilika haraka kwa wakati kabla mwaka mpya wa fedha haujaanza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili, alisema
katika ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Murya kikwazo ni Mwenyekiti wa kijiji
ambaye anazuia nguvu kazi za wananchi na kumhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba
atalishughulikia suala hilo na kasi ya ujenzi itaongezeka.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WILAYANI SINGIDA
No comments:
Post a Comment