Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mapokezi ya mradi wa kisima cha maji kwa wananchi wa kijiji cha Kihanju halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni.
Wananchi zaidi ya 2,000 wa Kijiji cha Kihanju Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni wameishukuru Serikali na Shirika la Water Aid kwa kuwajengea kisima cha kisasa cha maji ambacho kitasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji na kuimarisha shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.
Akihutubia wananchi wa Kijiji hicho leo baada ya uzinduzi na
makabidhiano ya mradi huo kwa jumuiya za watumia maji za Kijiji hicho Mkuu wa
Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka wananchi hao kushiri katika shughuli
za uendeshaji na matengenezo ya kisima hicho kwa kushirikiana na kamati za maji
za Kijiji hicho zilizoundwa ki sheria.
Hata hivyo RC Serukamba amewakumbusha wananchi hao kulipia
huduma za maji kwa wakati huku wakitakiwa kutunza vyanzo vya maji na kulinda
miundombinu isiweze kuharibika ili waendelee kunufaika na Mradi wa maji safi
kwa muda mrefu.
Aidha Serukamba amezitaka jumuia za maji kupanga bei za maji
kulingana na gharama za uzalishaji wa
maji hayo pamoja na kupanga mipango ya muda mrefu na mfupi ambayo itasaidia
kurejesha gharama za uendeshaji na matengenezo huku akikumbusha kuangalia uwezekano wa kulifikia kundi la
watu wasiojiweza ili waweze kupatiwa
maji.
Hata hivyo RC Serukamba ameagiza wananchi wa Kijiji cha
Kihanju kutumia uwepo wa maji hayo kujiongezea kipato kwa kufanya shughuli za
uzalishaji mali kwa kuwa wanatumia muda mfupi kupata huduma ya maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la vinywaji la
Serengeti SBL Mark Ocitti amesema mradi huo umegharimu kiasi cha Milioni 293.19
na utahudumia wakazi zaidi ya 2000 na kuendeleza shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi
wa hospitali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la vinywaji la Serengeti SBL Mark Ocitti akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi kisima.
Amesema kwamba Sekta ya kilimo katika maeneo hayo inategemewa
kukuwa kwa kiasi kikubwa kwakuwa kutakuwa na maji lakini pia uwepo wa muda wa
kutosha ambapo mashirika mbalimbali yatafanya uwekezaji kuongezeka.
Amesema kupitia programu za kijamii 2030 wametoa kipaumbele
katika utoaji wa ujuzi wa maisha kupita ufadhili wa masomo kwa wanafunzi
wanaosomea kilimo katika programu ijulikanayo kama Kilimo viwanda ambayo
imefadhili wanafunzi 200 tangu mwaka 2019.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba Kisima hicho
kitakuza shughuli za kiuchumi za kilimo ambazo zitachochea wataalamu wakubwa wa
Biashara ya Kilimo ambao watatoa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu za shayiri,
mtama na mahindi ambapo Shirika hilo limekuwa likinunu zaidi ya Tani 18,000 kwa
mwaka kutoka kwa wakulima.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA wilaya ya Manyoni Mhandis
Gabriel Ngongi amesema katika bajeti ya mwaka huu Mamlaka imetenga jumla ya TSH
Milioni 30 kwa ajilia ya kupelea maji katika vijiji vingine vitatu kutokea
Mradi ulipo.
Aidha ameushukuru ushirikiano uliofanywa na Shirika la water
Aid na Serengeti Breweries kwa mchango wao wa Kisima chenye uwezo wa Lita 7000
na pampu yenye uwezo mkubwa.
Awali akitoa Tathmini Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida
Mhandisi Lucas Said amesema mtandao wa maji mjini umefikia asilimia 78 wakati
mtandao wa maji Vijijini umefikia asilimia 61.
No comments:
Post a Comment