RAS huyo akaendela kusema kwamba, inapotokea mtumishi
amepata mafunzo ndani au nje ya nchi, ya muda mrefu au mfupi anapaswa kuonesha
ujuzi aliokuwa nao kwa kufanya kazi kwa umahiri ambapo anatakiwa kuwa
tofauti na wakati akiwa hajapata mafunzo
hayo.
Lengo la serikali la kumuongezea mtumishi maarifa ni
kumfanya awe na utendaji wa tofauti na awali na akawe mtumishi mwenye Tija, na ikatokea mtumishi hatimizi takwa
hilo atakuwa anaitia hasara serikali. alilisistiza Mwaluko.
Aidha RAS huyo akaendelea kufafanua juu ya zoezi la uchaguzi wa wafanyakazi hodari ambao
unatarajiwa kufanyika hivi karibuni na kuwataka wajumbe wa chama cha
wafanyakazi TUGHE kuhakikisha vigezo vya
kumpata mfanyakazi bora vinazingatiwa ili uhodari huo uweze kuonekana.
Dorthy ametoa wito kwa wajumbe wa baraza hilo na watumishi
wa Mkoa wa Singida kuchagua mtu kwa utendaji bora wa majukumu yake na isiwe ni
kumchagua kwa kuangalia sura au kuchaguana kwa zamu.
Naye Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Utawala na Rasilimali
watu Bw. Deogratius Yinza akijibu hoja
za wajumbe kuhusu kuongeza idadi ya watumishi na mpango wa mafunzo kwa mwaka
2022/23 amesema Serikali ina mpango wa kuajiri watumishi wa kada mbalimbali na
kubadilisha vyeo vya baadhi ya watumishi ili kuongeza tija.
Bwana Yinza akaendelea kubainisha kwamba tayari Mkoa
umekwishaanda mpango wa mafunzo kwa watumishi ambao ndio utakaotumika kutambua
aina ya watumishi na aina ya shule ambazo
mtumishi atakwenda .
Awali akiwapitisha wajumbe wa mkutano huo Kaimu Katibu
Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango na Uratibu Mkoa wa Singida Bi Beatrice
Mwinuka amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/23 mkoa umejiwekea vipaumbele
mbalimbali ikiwemo kuongeza makusanyo ya mapato kwa kuimarisha usimamizi na
udhibiti ili kuondoa mianya yote ya upotevu wa mapato.
Bi. Mwinuka amesema mkoa umedhamiria kuimarisha usimamizi na
ufuatiliaji ili Halmashauri ziwawezeshe wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya
wanawake na vijana.
Hata hivyo Mwinuka akaendelea kufafanua kwamba mwaka wa fedha 2022/23 mkoa wa singida
umeendelea kujipanga kuboresha mazingira ya uwekezaji viwanda vikubwa na vidogo
kutoka kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Aidha amebainisha kwamba mikakati hiyo inahusisha kuongeza
kiwango cha taaluma katika shule za Msingi na sekondari kwa kufanya ufuatiliaji
na usimamizi wa karibu kama sehemu ya kuleta mabadiliko makubwa ya elimu.
Akimalizia wasilisho lake Kaimu Katibu Tawala Msaidizi
Mipango na uratibu akaongezea kwamba
kwamba sekretarieti ya Mkoa wa Singida
katika kipindi cha mwaka 2022/23 imetenga jumla ya Tsh.Bilion 7.6
zitakazotumika katika matumizi mbalimbali ya mkoa.
Akifafanua kiasi hicho cha fedha Beatrice ameeleza kwamba
katika Tsh.Bilion 7.6 zilizotengwa kiasi
cha Tsh. Billion 5.02 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Tsh.2.78 ni
mishahara kwa ajili ya wafanyakazi wakati Tsh. Billion 2.23 ni kwa ajili ya
matumizi mengineyo.
Akizungumzia uendelezaji wa miradi ya maendeleo Bitrice
akaendelea kueleza kwamba mkoa umetenga Tsh.Bilioni 2.62 kwa ajili ya miradi
hiyo huku akibainisha kwamba kati ya
fedha hizo Tsh. Milioni 443.73 ni fedha za nje wakati fedha za ndani zikiwa
Bilioni 2.184.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha wafanyakazi TUGHE Mkoa
wa Singida Ethel Kahuluda akaipongeza sekretarieti ya Mkoa huo kwa kuweka
stahili mbalimbali za wafanyakazi katika bajeti zao na kuwasihi kwamba zitumike
kama zilivyopangwa
Katibu huyo akiendelea na pongezi hizo akamkumbusha muajiri kuhakikisha kwamba watumishi wanapata mafunzo stahiki ili kuboresha utendaji kazi wao huku akiwakumbusha watumishi kuyatumia mafunzo hayo kuleta mabadiliko chanya katika kazi zao.
Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekretarieti ya Mkoa wa Singida, Mtaalamu kutoka Sekretarieti ya Maadili, Makatibu Tawala wa wilaya za Manyoni Iramba, Singida vijijini, Manispaa ya Singida, ,Tughe, Wajumbe na Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Tughe.
No comments:
Post a Comment