Wednesday, January 24, 2024

RC SERUKAMBA AAGIZA KUKAMATWA WAZAZI WOTE WALIOFICHA WATOTO WALIOFAULI K...


Viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa Singida wametakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria Wazazi wote ambao hawajawapeleka watoto wao wenye sifa za kuanza Darasa Kwanza na wale wanaotakiwa kuripoti kuanza Kidato cha Kwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, alitoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kizonzo wilayani Iramba Mkoani humo.

Serukamba alisema ni lazima kila mtoto mwenyewe sifa za kuanza Darasa la Kwanza na wale waliofaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza wanaanza shule mara moja.

Alisema endapo mzazi au mlezi ataonekana kuwa kikwazo cha mtoto kuanza shule ni lazima achukuliwe hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani.

Aidha alisema kutokuwapeleka watoto shule ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata Elimu, ambayo kwa sasa serikali imeboresha miundombinu ya Elimu na kutoa elimu bila Malipo.

Hata hivyo Serukamba amewahimiza wananchi kuendelea kuutumia msimu huu wa Kilimo kuongea juhudi zaidiqq katika shuguli hizo za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa Mazao mbalimbali.

Alisema ili kuongeza uzalishaji wa Mazao, ni muhimu kwa wakulima kutumia Mbegu Bora na kuongeza matumizi ya Mbolea.

Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kizonzo walisema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma ya maji safi na Salama, hali inayowalazimu akina Mama kutembea umbali mrefu kufuata Maji kwa kutumia muda mrefu.

 

Kutokana na changamoto hiyo wananchi hao wameiomba serikali kuwapatia huduma ya maji kwa kusambaza maji katika vitongoji vyote vya kijiji cha Kizonzo.

Wananchi hao pia wameongeza kuwa kijiji hicho hakina Zahanati na kusababisha akina Mama na watoto kupata changamoto ya kufuata huduma za Afya umbali mrefu.

Walisema kukosekana kwa Zahanati kijijini hapo, imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa akina Mama wajawazito, hali inayosababisha baadhi ya akina Mama kujifungulia Njiani wakifuata Zahanati vijiji vya jirani.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kukagua ujenzi wa Zahanati kijiji cha Mukulu, kukagua ujenzi wa darasa moja shule ya msingi Mgongo, ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Sherui, Zahanati kijiji cha Mseko, amekagua ujenzi wa daraja la Mkima na Kituo cha Afya Mto Wilayani Iramba.


No comments:

Post a Comment