Maelekezo hayo yametolewa leo na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba wakati akisikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani hapo Mkutano ambao uliofanyika katika viwanja vya wazi katika Kijiji cha Puma.
Amesema vyombo vya Ulinzi na Usalama vishirikiane kupeleleza na kufanya msako mkali kuhakikisha watoto hao wanakamatwa na wanafunguliwa mashtaka ili kukomesha tabia hiyo huku akiwakumbusha wazazi kushirikiana na vyombo hivyo kuwapata.
Aidha, RC amekemea vikali tabia ya baadhi ya watu wanaoshiriki kuiba miundombinu ya barabara na umeme ambayo imesemekana inatumika kutengenezea mikokoteni na majembe ya kukokotwa na wanyama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho Samweli Mdimu ameelezea kero hiyo kwamba walifanya msako na kukamata baadhi ya watoto hao ambapo wazazi wao walikiri kwamba hawana pa kuwapeleka.
Samweli aliendelea kumueleza RC Serukamba kwamba walipowakamata na kuwafikisha Kituo cha Polisi Maafisa wa Polisi walishauri waachiwe kwa kuwa walikuwa na umri mdogo hivyo wazazi wao waelezwe ili wawaonye.
Aidha wananchi hao wameomba Polisi kuongeza ushirikiano na wananchi ikiwezekana kushirikiana na Mgambo wakati wa kufanya doria huku wakiomba Kituo chao cha Polisi kufanya kazi masaa 24 ili kiweze kuwasaidia nyakati zote.
Mwisho
No comments:
Post a Comment