Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Watumishi wa Mkoa huo wanaoshughulikia mambo ya ardhi kufanya kazi kwa weledi na kuwatendea haki wananchi ili kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi.
Kauli hiyo ameitoa leo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo wakati alipokutana na wananchi wenye kero mbalimbali ambapo alizisikiliza na nyingine kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha amewaasa watendaji wa Idara ya ardhi katika Manispaa ya Singida kufuata sheria na kuwatendea haki wananchi ili kuepuka uuzaji wa viwanja ambavyo tayari vinaumiliki wa watu.
Hata hivyo RC Serukamba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuchunguza malalamiko ya wananchi ambao wameuziwa viwanja ambavyo vina wamiliki zaidi ya mmoja pamoja na baadhi ya vituo vya Afya na zahanati ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kwa kuwauzia vifaa tiba na mambo mengine yenye hali ya ujinai.
Hata hivyo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uwazi na kuepuka kuonea watu kwa kuwa malalamiko mengi yanawataja watumishi wa umma.
"Katika kero zote zilizotolewa na wananchi ni dalili ya kwamba watumishi hatujafanya kazi yetu vizuri, wananchi bado hawajapewa elimu ya kutosha kwa hili tunatakiwa kubadilika " Serukamba.
Zoezi la kuwasikiza wananchi litaendelea kesho katika Wilaya ya Ikungi
Mwisho
No comments:
Post a Comment