Thursday, August 11, 2022

Mwenge wa Uhuru Watua Singida Vijijini

Mwenge wa Uhuru umefikisha siku ya Tatu Mkoani Singida na leo umekabidhiwa Wilaya ya Singida Vijijini katika viwanja vya Kihonda ambapo walibainisha kwamba Mwenge wa Uhuru utakimbizwa km 130 Wilayani hapo.

Akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amesema Mwenge wa Uhuru utakagua Miradi mitano na prodramu Tano katika maeneo mbalimbali ya eneo hilo.

DC Muragili amesema programu hizo zinahusiana na kupinga Rushwa, Mapambano dhidi ya Malaria, mapambano dhidi ya UKIMWI/VVU na Lishe Bora kwa wananchi.

Aidha Muragili amesema programu hizo zinalenga kuondoa viwango vya maambukizi ya UKIMWI na Malaria ambayo kwa Mkoa wa Singida ni asilimia 2.3 ikilinganishwa na asilimia 7.3 ya maambukizi ya Malaria ki Mkoa.

Kwa upande wake Mratibu wa Malaria Wilaya ya Singida Bwana Mafanikio Mamba amesema Wilaya imechukua hatua kadhaa kupambana na Ugonjwa wa Malaria kwa nia ya kupunguza maambukizi hasa kwa mama wajawazito.

Amesema kwa mwaka 2021/22 watu 25,589 walipima Malaria ambapo wanaume walikuwa 9369 wanawake ni 16,220 na kubainika kwamba watu 451 walikuwa na vimelea vya Malaria.

Aidha Halmashauri ya Singida imegawa  vyandarua 25,000 sawa na robota 625 kwenye huduma za kutolea huduma kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano alisisitiza Bwana Mafanikio.

Wilaya ya Singida Vijijini imeendelea kutoa elimu ya kujikinga na maagonjwa ya kuambukiza jkiwemo ukimwi ambapo programu ya VVU/UKIMWI Singida ina vituo 37 vinavyotoa huduma ya ushauri nasaha na upimaji.

Kwa mujibu wa Mratibu wa UKIMWI wa Wilaya hiyo amesema jumla ya watu waliopima VVU katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021 ni 45162  kati yao wanaume ni 18251 sawa na asilimia 40 na wanawake walikuwa ni 26911 sawa na asilimia 60.

Hata hivyo Mwenge wa Uhuru utaendelea na  ukaguzi wa miradi ya maendeleo kesho Agosti 12, 2022 Singida Mjini.

No comments:

Post a Comment