Sunday, July 17, 2022

WAHANDISI MKOANI SINGIDA WAMKOSHA WAZIRI MKUU

Muenekano wa daraja la Mkomo lililopo  Kata ya Iguguno Wilayani Mkalama


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwapungia mikono wananchi wa kijiji cha Mkomo waliohudhuria ufunguzi wa daraja hilo hafla iliyofanyika leo 17.07.2022 katika eneo hilo
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge wakata wa ukaguzi wa daraja la Mkomo uliofanyika leo 17.7.2022 katika kijiji cha Mkomo wilayani Mkalama


Mhandisi wa TARURA Mkoani Singida Tembo David akimuonesha waziri mkuu mchoro iliyotumika katika ujenzi wa daraja la Mkomo
Waziri Mkuu akiendelea kupata maelezo kutoka kwa Mhandisi Tembeo


ukaguzi wa daraja unaendelea
Baadhi ya wahandisi wa Mkoa wa Singida baada ya kupongezwa na waziri mkuu
wahandisi wa Mkoa wa Singida wakiwa na waziri mkuu 

wahandisi wa Mkoa wa Singida wakiwa na waziri mkuu 



Waziri Mkuu wa Jamhuri muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewapongeza wahandisi wa Mkoa wa Singida kwa umahiri wao Katika kubuni na kusimamia kazi za Ujenzi ambazo zimefanyika sehemu mbalimbali Mkoani hapo.

Pongezi hizo zimetolewa leo Katika Kijiji Cha Mkomo kilichopo kata ya Iguguno Mkoani hapo wakati wa ukaguzi wa daraja la Mkomo ambapo wahandisi kwa kutumia ubunifu wao wameweza kuokoa Milioni 448 Katika Ujenzi wa daraja hilo kwa kutumia teknolojia rahisi ya mawe.
Waziri Mkuu amesema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga madaraja ambapo endapo teknolojia hiyo itaenezwa kwa wahandisi wengine itazidi kuokoa fedha nyingi za Serikali katika Ujenzi huo.
"Nawapongeza Sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, nimetembelea Ujenzi wa shule ya wasichana Solya wilayani Manyoni, nimetembelea Kituo Cha Afya Mtoa Iramba leo nipo Mkomo nimeiona daraja la mawe nawapongeza kwa kazi nzuri na ubunifu mnaofanya, mmeokoa kiasi kikubwa Cha fedha" alisema
Amesema umefika wakati sasa wahandisi wengine kuiga taaluma hiyo ya mawe kwa kila Mkoa kwakuwa kila Mkoa una mawe mengi Jambo ambalo litasaidia kupunguza gharama za Ujenzi.
Amewataka wahandisi hao kwenda kuangalia eneo la Mtoa Wilayani Iramba na kufanya tathmini ya unenzi wa daraja kubwa Katika eneo lenye usumbufu wa maji ambapo Awali ilionekana kujitaji gharama za TSH. Milioni 900.
" nataka wahandisi wa mikoa mingine waige ili tuweze kujenga madaraja ya mawe, Lakini pia Jana wananchi wa kata ya Mtoa waliomba Serikali kuwajengea daraja katika kata hiyo,Sasa nendeni mkafanye tahamni kwa kuwa inawezekana tukapunguza gharama kutoka Milioni 900 mpaka kufikia Milioni 102"alisema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake Mhandisi wa TARURA Tembo Devidi ambaye ndiye Msimamizi wa Ujenzi wa daraja hilo la Mkomo amesema daraja limekamilika kwa asimia mia moja na limegharimu sh.102 kwa kutumia teknolojia ya mawe na endapo lingetumia lingegharimu Milioni 550.
Amesema daraja hilo lenye urefu wa Mita 30 na upana wa Mita 7 litawasaidia wananchi kuendesha Shughuli mbalimbali zikiwemo Biashara na huduma nyingine kijamii.
Amesema teknolojia hiyo ya mawe imetumika zaidi katika nchi za Hispania na kwa hapa Nchini zaidi ni Mkoa wa njombe na Kigoma
Naye Naibu Waziri wa TAMISEMI Dr.Festo John Dugange Wameendelea kuwasiliana na meneja TARURA wa Mikoa kuahakikisha babara zinakuwa Bora na za viwango vya juu na zipitika kwa mwaka mzima.
Amesema Katika mwaka wa fedha wa 2022/23 walaya ya Mkalama imeongezewa bajeti ya Barabara za TARURA kutoka mioni 600 hadi kufikia Bilioni 2.2 Lengo likiwa ni kuboresha Maisha ya wananchi wakati bajeti ya Mkoa wa Singida ikiwa imeongezewa kutoka Bilioni 6 mpaka Bilioni 23.
Mwisho

No comments:

Post a Comment