Mmoja
wa majeruhi akipatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara
baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
Mmoja
wa majeruhi akiwa amelazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu ya mkono katika
hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6
katika kijiji cha Kijota, Singida.
Baadhi
ya ndugu na jamaa wa majeruhi wa ajali ya lori iliyoua watu sita wakiwa nje ya
wodi za wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.
Watu
sita wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye namba za
usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa (39) mfanyabiashara
mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha
Kijota, Singida.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea Agosti
27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota wakati likitokea
mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini.
ACP
Magiligimba ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori hilo Jumanne
Kidanka (32) Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa
dereva ambaye hakuwa makini akiwa anaendesha lori hilo lililosheheni abira na
mizingo mingi.
Amewataja
waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi Mohammed (40)
wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30) mkazi wa kijiji cha
Mwakiti.
ACP Magiligimba
amewataja wengine kuwa ni Allen Mwangu (38) mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas
Stephano (40) mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari (19) mkazi wa kijiji
cha Ilongero.
Ameongeza kuwa
majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi wamelazwa
hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa
katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.
Ameeleza
kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku wengine
waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya miili yao.
“Hawa
wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini Singida,
Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote wamevunjika miguu. Miili
ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali misheni Mtinko”, amesema.
No comments:
Post a Comment