Mkuu wa Wilaya ya
Singida Elias Tarimo akizungumza katika kikao na wataalamu watakaofanya
uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la
Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mthamini wa ardhi
kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Chiku Mkina (aliyevaa miwani) na watalaamu wengine wakisikiliza kwa makini
mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika
mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Katibu Tawala Mkoa wa
Singida Dkt Angelina M Lutambi akichangia mada katika kikao kilichohusu
uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la
Kutoka Uganda hadi Tanga.
Wananchi Mkoani Singida
wameondolewa wasiwasi kuhusu fidia ya mali au ardhi yao ambayo itapitiwa na
mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga kwakuwa hawatapunjwa bali itazingatia
vigezo vya kimataifa na kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya
Singida Elias Tarimo amesema hayo mapema leo wakati wa kikao na wataalamu
wanaofanya uthamini wa mali na ardhi ambayo itapitiwa na mradi huo.
Tarimo amesema
wananchi na taasisi zote wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutaja gharama
kulingana na thamani halisi ya mali zao na sio kuongeza gharama za juu kwakuwa
vigezo vya kitaifa na kimataifa vitazingatiwa.
“wananchi wengine
wasio waaminifu wananweza wakataja pesa kubwa au hata kuvamia maeneo ambayo
siyo yao ilimradi wapate tu pesa, nawasihi wasifanye hivyo kwakua watakuwa
wanakwamisha mradi huu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu na majirani zetu
Uganda”, amesema na kuongeza kuwa
“ Tunampongeza na
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John P Magufuli kwa
kuhakikisha nchi yetu inapata mradi huu, tutoe ushirikiano wa kutosha ili mradi
ufanikiwe kw kiwango kikubwa hasa kwa maeneo yote utakapopita kwa Mkoa wa
Singida”, amesisitiza.
Tarimo ameongeza kuwa
serikali ya Mkoa, wilaya, taasisi na wananchi wote wa Singida wamekuwa mstari
wa mbele kutoa ushirikiano kwa miradi yote ya kitaifana kimataifa na hivyo basi
wataalamu wanaofanya uthamini na wale watakaokuja kujenga wasiwe na wasiwasi
wowote.
Ameongeza kuwa
wananchina taasisi ziko tayari kunufaika na mradi huo kupita Mkoani Singida kwa
kupata ajira za muda mfupi na mrefu, kufanya biashara pamoja na kutoa huduma
mbalimbali.
Kwa upande wake
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina M Lutambi amewataka wataalmau hao
kushirikiana na wataalamau wa ngazi zote kuanzia mkoa hadi vijiji ili zoezi la
uthamini liende vizuri.
Dkt Lutambi amesema
lengo la uthamini ni kuhakikisha wananchi hawapati madhara makubwa kutokana na
kupita kwa mradi huo katika maeneo hayo pamoja na kuhakikisha sheria, miongozo
na taratibu zote zinafuatwa.
Ameongeza kuwa
wataalamu wanapaswa kuwa wazi kwa kushirikisha taasisi na mashirika ambayo kwa
namna moja au nyingine yataguswa na mradi huo pamoja na kutoa taarifa sahihi na
kwa wakati kwa wote wanaohusika.
Wakichangia mada
katika kikao hicho wataalamu kutoka Mkoa wa Singida wamesema uthamini uangalie athari
zote ambazo zinaweza kutokea kutokana na mradi huo mfano athari ya kisaikolojia
ya usumbufu wa kumhamisha mtu kutoka katika makazi yake pamoja na thari za
maeneo kama vyanzo vya maji ambapo bomba litapita.
Mkurugenzi wa kampuni
ya Dighy Welly Dkt Jan Perold akiwasilisha mada katika kikao kilichohusu
uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la
Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mwakilishi wa
Serikali katika zoezi la Uthamini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Linus
Kinyondo akizungumza na wataalamu wa mkoa wa Singida katika kikao kilichohusu
uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la
Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mhandisi wa Ujenzi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Simwela Nuru Martin akifuatilia kwa makini kikao
kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba
la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
No comments:
Post a Comment