Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Manju Msambya wakikagua moja ya jengo la maabara ya sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V.
Kone ameitaja Wilaya ya Ikungi kuwa ya mwisho katika ujenzi wa vyumba vitatu
vya maabara kwa kuwa kati ya sekondari 30 za wilaya hiyo hakuna hata moja
iliyofikia hatua ya kupaua majengo hayo.
Dkt. Kone ameyasema hayo mapema wiki
hii wakati wa ziara ya siku mbili Wilayani humo ya kukagua ujenzi wa vyumba vya
maabara za shule za sekondari.
Amesema viongozi na watendaji wanapaswa
kuhamasisha, kukusanya na kusimamia matumizi sahihi ya michango ya wananchi
ikiwemo ya ujenzi wa maabara za sekondari.
Aidha Dkt. Kone ameongeza kuwa
watendaji na viongozi wilayani humo waache kulalamika kuhusu wanasiasa
wanaopotosha wananchi juu ya uchangiaji wa maendeleo yao bali wachukue hatua za
kisheria wanapokuwa na ushahidi.
Dkt. Kone amesisitiza ujenzi wa maabara
kwa kuwa una manufaa makubwa kwa jamii kwa kupata wanasayansi na wagunduzi
wengi wazalendo, pia nchi itaongeza idadi ya waalimu ya sayansi, madaktari,
wahandisi na wanasayansi wa kada mbalimbali.
Amezishauri
Serikali za vijiji kuweka sheria ndogo ndogo zitakazo saidia katika kukusanya
michango ya maendeleo ikiwemo utaratibu wa kuwawajibisha wale wasiochangia.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone akikagua moja ya jengo la maabara ya sekondari wilayani Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Manju Msambya akitoa ushauri kwa watendaji na viongozi juu ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara ya sekondari (pembeni yake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone).
Baadhi ya Watendaji na viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone wakati wa majumuisho ya ziara yake Wilayani humo.
No comments:
Post a Comment