Monday, September 15, 2014

WAAJIRIWA WAPYA MKOANI SINGIDA WAFUNDISHWA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA.

Watumishi waajira wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.
 
Waajiriwa wapya 22 wa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida wameaswa kutotamani utajiri wa haraka katika utumishi wao serikalini bali wazingatie maadili ya utumishi wa umma.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan amewataka watumishi hao kujituma na kuendeleza sifa bora ya Mkoa wa Singida ya kufanya vizuri katika utendaji kazi.

Hassan amesema serikali ndiye mwajiri Mkuu kwa sasa kwani hutoa ajira kwa watu wengi na ajira ya serikalini ni mahali pazuri pa kufanyia kazi.

Kaimu Mhasibu Mkuu Melchior Rweyemamu (aliyesimama) akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan kufungua semina fupi kwa waajiriwa wapya, semina hiyo imeandaliwa na ofisi ya Uhasibu.

Naye Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa Wilbard Marandu amesema Mkoa wa Singida umeendelea katika sekta za uchumi, mawasiliano, barabara, afya na maji hivyo kuufanya mji huo kuwa mahali pazuri pa kazi.

Ameongeza kuwa waajira hao wanapaswa kuwa na mtazamo wa kuwahudumia wananchi kupitia utumishi wao serikalini na si kupata utajiri wa haraka.


























Baadhi ya watumishi waajira wapya wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.

























Mwajiriwa Mpya Mhasibu Msaidizi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida  Esther Kiria akimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.

























Watumishi waajira wapya (waliochuchumaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.

No comments:

Post a Comment