Thursday, August 14, 2014

MKUTANO WA KANDA YA KATI WA WADAU WA MAENDELEO KUTOKA MAENEO KAME WAFANYIKA MJINI SINGIDA.


Wadau wa Maendeleo kutoka Kanda ya kati (Dodoma, Tabora na Singida) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan (katikati) Mgeni rasmi wa Mkutano uliojadili changamoto na fursa za Mikoa yenye Ukame katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi Kulia kwake ni Prof. Claude Mung'ong'o na kushoto ni Prof. Faustin Maganga kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 



Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan akifungua mkutano wa kikanda wa wadau wa maendeleo kutoka maeneo kame kanda ya kati uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Singida.

Mtafiti mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Claude Mung'ong'o akitoa maelezo kuhusu maeneo kame yaliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi.
 

Wadau wa maendeleo wakifuatilia mkutano kuhusu fursa na changamoto za Mikoa yenye ukame ya Kanda ya Kati kutokana na mabadiliko ya tabianchi.


Katibu Tawala wa mkoa Singida Bw. Liana Hassan na Prof. Claude Mung'ongo (kulia) wakifuatilia mkutano kuhusu fursa na changamoto za Mikoa yenye ukame ya Kanda ya Kati kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan akizungumza katika mkutano wa kikanda wa wadau wa maendeleo kutoka maeneo kame kanda ya kati uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Singida.


Picha kwa hisani ya 'Centre for Climatic Change Studies, University of Dar es Salaam'.

No comments:

Post a Comment