Dendego, ametoa kauli hiyo leo (19
Aprili, 2024) katika Kijiji cha Kashangu, Halmashauri ya Itigi kwenye ziara
yake ya kikazi ya Siku Mbili kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya
Elimu na Afya.
Aidha ameonya kuwa hatasita
kuwachukulia hatua Viongozi wa Vijiji na Kata ambao watashindwa kudhibiti hali
hiyo ya unywaji wa pombe nyakati za asubuhi badala ya kuhimiza wananchi kwenda
kufanya shughuli halali za kijitafutia riziki.
“Mnaanza kunywa Pombe asubuhi hasa watoto wa kike hii Sio sawa lazima
tusimamiane nikikuta jambo linaenda ndivyo sivyo nitakamata Mtendaji kwa sababu
anasheria kama zangu na kwanini ashindwe kudhibiti vitendo hivyo
tutawajibishana vikali,” Amesisitiza RC Halima Dendego.
Kuhusu utoaji wa chakula mashuleni,
amewaagiza Wakuu wa Shule zote za Mkoa wa Singida kwa ushirikiano na Viongozi
wa Vijiji na Kata kuweka utaratibu wa kutoa chakula kwa wanafunzi ili
kuhakikisha wanajifunza kwa bidii.
Amesema utoaji wa chakula mashuleni
utasaidia kwa kiasi kikubwa kupandisha ufauli kwa wanafunzi hivyo ni muhimu kwa
kila shule kuanza utaratibu wa kutoa chakula kwa wanafunzi wao.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa
wa Singida Dkt. Fatuma Mganga amewataka Watendaji wa Halmashauri na Kata Mkoani
humo kusimamia vizuri ujenzi wa miradi ya maendeleo hasa umaliziaji wa majengo
mbalimbali ili kudhibiti vitendo vya wizi wa vifaa vya ujenzi.
Amesema hatapenda kusikia wala
kuona wizi wa vifaa katika miradi ya maendeleo hivyo Viongozi lazima wasimamie
kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora
ambao utaleta manufaa kwa Wananchi na sio vinginevyo.
Katibu
Tawala huyo wa Mkoa amesema kumekuwa na tabia ya kuiba vifaa hasa vinapopelekwa
kwenye miradi ya maendeleo jambo ambalo linasababisha utekelezaji wa baadhi ya
miradi kujengwa chini ya kiwango na kusisitiza kuwa tabia hiyo itakoma iwapo
Viongozi wote watashirikiana katika ngazi zote.
Ziara hiyo ya Siku mbili ya Mkuu wa Mkoa huo itaendelea kesho (tarehe 20 Aprili, 2024) ambapo atakagua Ujenzi wa nyumba ya Walimu katika Shule ya Sekondari Kitaraka, Kihanju kukagua Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Itigi pamoja na kusikiliza na kuzitatua kero za wananchi wa Halmashauri hiyo ya Itigi mkutano utakaofanyika katika ofisi ya kijiji cha Songambele.
No comments:
Post a Comment