Friday, December 01, 2023

RAS SINGIDA AKEMEA TABIA YA UKATILI, WANAWAKE NA WATOTO.

Wakati Dunia ikipiga vita tabia ya ukatili dhidi ya binadamu, takwimu zinaonesha kuwa wanawake wenye umri miaka 15 hadi 49 waliofanyiwa ukatili wa kingono kimwili na kihisia na wenza wao Mkoani Singida ni asilimia 45.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga amesema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa ‘Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia’, kwa wajumbe wa mpango kazi wa Taifa juu ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto waliokutana ukumbi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Singida wenye kauli mbiu ya “Wekeza: Kuzuia Ukatili wa Kijinsia’’.

“Mpango kazi huu ulitengenezwa kwa njia shirikishi na ninayo imani kubwa kuwa kupitia mpango huu kila mdau atatambua wajibu wake na kuutekeleza ili tufikie malengo tuliyojiwekea ya kutokomeza ukatili dhidi wa wanawake na watoto kwa asilimia 50, ifikapo 2028,” alisema.

Aidha Dkt. Mganga alibainisha kuwa utafiti uliofanywa nchini na (The 2009 National Survey on Violence against Children), unaonesha asilimia 28 ya wasichana na wavulana asilimia 13, wamefanyiwa ukatili wa kingono katika mazingira ya nyumbani.

Aidha Dkt. Mganga alisema asilimia 73 ya wasichana na asilimia 72 ya wavulana wamefanyiwa ukatili wa kimwili na zaidi ya asilimia 60, wakibainika kufanyiwa na ndugu wa karibu huku wengine asilimia 40, hufanyika wakiwa shuleni.

“Hata hivyo utafiti huu unaonesha kuwa robo ya watoto wa kitanzania wakiwemo wavulana na wasichana wamefanyiwa ukatili wa kihisia au kisai   kolojia…,” alifafanua Dk. Mganga.

Katibu Tawala huyo alisema kuwa, kupitia siku 16 za kupinga Ukatili wa Kinjinsia kwa mwaka 2023,  iwe chachu kwa jamii kubadili sura  ya vitendo vya ukatili, katika nchi na hasa Mkoa wa Singida, ambao upo kati ya Mikoa ambayo   Mimba, ndoa za utotoni na ukeketaji bado ni changamaoto kubwa.

Katika kuhakikisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili yanafanikiwa, Dk. Mganga aliwataka wajumbe wa kamati ya….., wakatoe elimu kwenye taasisi na makundi mbalimbali, na kuwasilisha taarifa siku ya kilele, novemba 10, 2023, juu ya namna wajumbe walivyotekeza kampeni hii.

Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ni kampeni kabambe ya kimataifa, inayosimamiwa na kituo cha kimataifa cha Wanawake, tangu mwaka 1991, katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa na kuleta matokeombora kwa jamii.

No comments:

Post a Comment