Thursday, October 13, 2022

DC MWENDA ASHANGAZWA NA WANAOSEMA HALMASHAURI YA IRAMBA HAIJAWACHUKULIA HATUA WALIOFUJA FEDHA ZA UMMA

 

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa za upotoshaji zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba Halmashauri ya Wilaya hiyo haijawahi kuchukua hatua kuhusu ufujwaji wa fedha za makusanyo ya mapato uliofanywa na baadhi ya Watumishi na Mawakala wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza jana katika ukumbi wa mikutano mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Tume ya Mahakama uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida DC huyo amesema mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo walianza kuchukua hatua kwa kushirikiana na viongozi wengine ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi waliohusika.

Aidha alibainisha kwamba jumla ya Watumishi 72 walikusanya fedha na hawakuzipeleka katika akaunti ya Halmashauri ambapo walipelekwa TAKUKURU ili uchunguzi ufanyike ikiwezekana wachukuliwe hatua.

DC Suleiman aliendelea kueleza kwamba baada ya hatua hiyo Watumishi 49 kati ya Watumishi 72 wameshalipa madeni yao kiasi cha Tsh.Milioni 93

“Aidha  tarehe 28 July niliagiza watu 18 kati ya watumishi 72 kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi na itakapobainika kutumia fedha  hizo waweze kuchukuliwa hatua”. Aliendelea kufafanua DC wa Iramba

Hata hivyo tuliunda kamati ya uchunguzi ambayo iliwaita na kuwahoji bàadhi ya Watumishi hao ambapo majina yao yalipelekwa kwenye Baraza la Madiwani ili kuhojiwa zaidi.

Baada ya mahojiano na Baraza la Madiwani ilibainika kwamba  watumishi hao walikusanya fedha hizo na kizitumia hivyo ikaamuliwa kuwafukuza kazi watumishi sita (6) huku wakiwapa Watumishi 11 siku 45 kurejesha fedha hizo na endapo wakishindwa wataungana na wezao waliofukuzwa alieleza DC Suleiman

Moja kati ya waliofukuzwa kazi ni Afisa biashara wa Wilaya  Prosper Banzi huku kupeleka  Muweka Hazina wa Halmashauri (Muhidini) kupeleka  TAKUKURU pamoja na watumishi wengine wanne kwa ajili  ya mahojiano na kesi zao zinaendelea.

Hata hivyo ameeleza muandishi kuandika kwamba hakuna hatua iliyochukuliwa katika Halmashauri hiyo sio sahihi na huenda ana lengo la kuwachonganisha viongozi wa Serikali na wananchi wake.

"Hata hivyo bado mwandishi huyo alikuwa na nafasi ya kubalansi story yake kwa kuuliza viongozi wa Halmashauri hiyo kama kuna hatua iliyochukuliwa". Alieleza DC

Aidha Mwenda amesema inawezekana mtu huyo aliandika habari kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa huenda anatumiwa na wale ambao wamewafukuza.

"Tutaendelea kuwa wakali na tutaendelea kuchukua hatua stahiki bila kumuonea mtu” alisema Mwenda


No comments:

Post a Comment