Thursday, May 15, 2014

UGENI WA WATOTO WA MFALME NA MACHIFU KUTOKA SWAZILAND.


























Watoto wa Mfalme kutoka Swaziland wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone na Katibu Tawala Mkoa Liana Hassan nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone amepokea ugeni wa Viongozi 22 kutoka Swaziland ambao wako katika mafunzo juu ya uhifadhi wa ardhi na maliasili nchini Tanzania.

Dkt. Kone amepokea ugeni huo uliojumuisha watoto wa mfalme na mchifu kutoka Swaziland ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lubombo nchini humo Sylvia Mthetwa na kuzungumza nao kuhusu uhifadhi wa maliasili Mkoani Singida.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Lubombo Swaziland Sylvia Mthetwa akizungumza na viongozi kutoka Swaziland (hawapo pichani).

Viongozi hao walitaka kufahamu kuhusu umiliki wa ardhi, hatua zilizochukuliwa na Mkoa katika kutunza maliasili hasa misitu, na mazao yaliyopo Mkoa wa Singida.

Katibu Tawala Mkoa Liana Hassan akitoa maelezo kuhusu uhifadhi wa maliasili Mkoani Singida kwa viongozi kutoka Swaziland pemben yake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone.

Wakiwa Mkoani Singida viongozi hao wametembela Msitu wa Aghondi uliopo Wilaya ya Manyoni, pia wametembelea Mkoa wa Morogoro katika Chuo Kikuu cha Sokoine na Mkoa wa Shinyanga.


Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Aziza Mumba akitoa maelezo juu ya taratibu za uhifadhi wa Misitu kwa Viongozi kutoka Swaziland.

 Viongozi kutoka Swaziland wakiingia katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Wa kwanza ni Mtoto wa Mfalme akiwa na viongozi kutoka Swaziland wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment