Serikali imesema inaendelea na mchakato wa kufungua
miundombinu mbalimbali ikiwemo njia ya reli kutoka Manyoni hadi Singida ili
kusaidia kukuza uchumi na kurahisisha mawasiliano baina ya Mkoa huo na maeneo
mengine ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 30.10.2022 na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani katika ibada ya kuwekwa wakfu
Askofu Syprian Hilinti wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, hotuba iliyosomwa
kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba.
Serukamba amesema mchakato huo unaendelea kutokana na maombi
yaliyofanywa awali na Kanisa hilo ambapo Serikali ya mkoa imewasiliana na
Shirika la reli TRC ambapo bado wanaendelea tathmini za kufungua njia hiyo.
Akiendelea na hotuba RC Serukamba amesema ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa Mkoani hapa upo katika mpango wa Serikali ambapo Mkoa ulipokea maelekezo ya kubainisha eneo la uwanja utakapojengwa.
Hata hivyo ilibainika kwamba eneo la uwanja wa ndege wa sasa limevamiwa na kujengwa nyumba za makazi jambo ambalo linaunyima sifa uwanja huo kutengenezwa kwa hadhi na kiwango cha kisasa alieleza Serukamba.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisoma hotuba katika ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Syprian Hilinti wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati iliyofanyika Singida mjini.
"Eneo la pili lililobainishwa na kutengewa Kijiji cha
Manga linahitaji malipo makubwa ya fidia ili wananchi waliomo ndani ya eneo
hilo wapishe kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege" alieleza RC Serukamba
Aidha RC Serukamba amefafanua kwamba barabara ya Singida –
Hydom - Mbulu ipo kwenye mpango na utekelezaji wake umeanza ambapo kipande cha
Singida - Ilongero - Hydom chenye urefu wa KM 93.3 kazi ya upembuzi yakinifu na
maandalizi ya kutangaza zabuni zinaendelea na uthamini katika barabara hiyo
umekwisha fanyika.
Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Syprian Hilinti wa Kabisa la KKKT Dayosisi ya Kati ikiendelea.
No comments:
Post a Comment